Joy FM

Viongozi CCM watakiwa kuwekeza kwa watoto

8 January 2024, 14:20

Viongozi wa umoja wa  UVCCM  Kata ya Gungu Manispaa ya Kigoma Ujiji wameomba viongozi wa chama hicho Mkoa wa Kigoma pamoja na wananchi kuwekeza katika malezi ya watoto kwa kuwalea katika misingi ya uadilifu ili baadaye waweze kulitumikia taifa na kuleta maendeleo.

Na, Lucas Hoha

Vijana hao wametoa ushauri huo ikiwa ni baada ya kupokea msaada kwa ajili vijana wa chipukizi na baadhi ya kaya zilizoathiriwa na mvua zinazoendelea kunyesha kutoka kwa madiwani wa Viti maalumu katika Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Wamesema pindi watoto wanapolelewa katika maadili ya taifa lao wanakuwa wazalendo na kueleta maendeleo chanya kwa wananchi

Nao madiwani wa viti maalumu ambao wametoa msaada huo ambao ni Zabibu Mtende na Shumbana Kassim wamesema maendeleo ya taifa la Tanzania hayawezi kupatikana kama viongozi watashindwa kuwalea watoto katika maadili,

Kata ya Gungu ni miongoni mwa maeneo hapa Mkoani Kigoma ambayo yameathiriwa na mvua zinazoendelea kunyesha huku ikiacha uharibifu wa mali za watu na miundombinu mbalimbali.