Joy FM

Mwanafunzi darasa la 6 Kigoma abuni ‘Earphone’

11 November 2024, 08:43

Selemani  Mathias mwanafnzi wa darasa la sita shule ya Msingi Kigoma akionyesha alivyobuni Ear phone zenye Redio, Picha na Joy FM

Wadau wa maendeleo wametakiwa kushirikiana na kuendeleza bunifu mbalimbali za watoto ili waweze kufikia ndoto zao kwa manufaa ya jamii na Taifa kwa ujumla.

Na Timotheo Leonard – Kigoma

Novemba 10 ya kila mwaka dunia huadhimisha siku ya sayansi ambayo hufanyika ili kuonyesha bunifu mbalimbali kutoka kwa wabunifu wakubwa na wanaochipukia ambapo  wazazi na walezi Mkoani Kigoma wameaswa kutambua na kukuza ubunifu wa watoto wao kwa lengo la kukuza vipaji vyao.

Siku ya Sayansi duniani kwa amani na maendeleo ilitangazwa rasmi na UNESCO mwaka 2001 ikiwa na umuhimu wa sayansi katika maisha ya kila siku na hitaji la kushirikisha  umma masuala ya kisasa yanayohusiana na sayansi ikiwemo ubunifu

Mtangazaji wa Redio Joy Fm, Bi. Elisheba Ndijenyene akiwa amevaa headphone zilizobuniwa na mwanafunzi wa drasa la sita

Licha ya siku hii kuadhimishwa kila mwaka wapo baadhi ya wazazi ambao huwachukua muda mrefu kuelewa vipaji vya watoto na kuviendeleza kama anavyosema Scander Kassim baba mzazi wa Selemani Mathias ambaye mwanae ametengeneza Ear phone zenyewezo wakushika stesheni zote za Redio.

Sauti ya Scander Kassim baba mzazi wa Selemani Mathias ambaye mwanae ametengeneza Ear phone

Selemani  Mathias ni mwanafnzi wa darasa la sita shule ya Msingi Kigoma hapa anatueleza alivyobuni Ear phone zenye Redio.

Sauti ya Selemani  Mathias ni mwanafnzi wa darasa la sita shule ya Msingi Kigoma

Bi. Genoveva Emmanel Mtiti ni Mkurugenzi wa Veva Craft lakini pia ni Mratibu wa siku ya sayansi duniani kwa Mkoa wa Kigoma anasema siku ya Novemba 10 mwaka huu zaidi ya  watoto 500 watahudhuria maadhimisho hayo kutoka halmashari zote  huku watoto 30 wakitarajiwa kuonyesha ubunifu wao.

Sauti ya Bi. Genoveva Emmanel Mtiti ni Mkurugenzi wa Veva Craft