Joy FM

Makarani wa uchaguzi watakiwa kuwa wadilifu Kasulu

28 May 2026, 13:21

Makarani waongozaji wapiga kura wakipatiwa mafunzo ya uchaguzi ili kusimamia uchaguzi katika kata ya Nyumbigwa, Picha na Hagai Ruyagila

Uchaguzi ni msingi muhimu wa demokrasia katika nchi yoyote na kupitia uchaguzi, wananchi hupata nafasi ya kuchagua viongozi wanaowataka kwa hiari yao

Na Hagai Ruyagila

Makarani waongozaji wa wapiga kura katika uchaguzi mdogo wa Madiwani kata ya Nyumbigwa Jimbo la Kasulu mjini mkoani Kigoma, wametakiwa kuwa waadilifu na kuepuka kuwa chanzo cha migogoro kwa vyama vya siasa.

Wito huo umetolewa na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kasulu Mjini, Nurfus Aziz Ndee, wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa makarani hao ambapo amewataka kuzingatia sheria na kanuni za tume huru ya taifa ya uchaguzi.

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kasulu Mjini, halmashauri ya Mji Kasulu, Nurfus Aziz Ndee, Picha na Hagai Ruyagila

Aziz amewasisitiza wasimamizi hao kutoa kipaumbele kwa watu wenye mahitaji malumu ili wapate haki ya kuchagua kiongozi wanayemtaka.

Sauti ya Nurfus Aziz Ndee

Baadhi ya makarani waongozaji wapiga kura ambao wameshiriki mafunzo hayo wamesema semina hiyo imewasaidia kuongeza uelewa kuhusu majukumu yao pamoja na namna ya kusimamia uchaguzi kwa uhuru na haki.

Sauti ya Makarani waongozaji

Uchaguzi mdogo wa madiwani unatarajia kufanyika jumatatu ya tarehe 1 mwezi wa sita mwaka huu, hii ikiwa ni kufuatia kifo cha aliyekuwa diwani wa kata Nyumbigwa kupitia chama cha mapinduzi CCM.

Makarani waongozaji wapiga kura wakipatiwa mafunzo ya uchaguzi ili kusimamia uchaguzi katika kata ya Nyumbigwa, Picha na Hagai Ruyagila

Hata hivyo jumla ya makarani 23 wamepatiwa mafunzo hayo.