Joy FM

Wahitimu kidato cha sita waaswa kuwa na maadili mema Kasulu

30 April 2026, 10:23

Wanafunzi wa kidato Cha sita katika shule ya sekondari Kasulu, Picha na Hagai Ruyagila

Maadili mema ni mwongozo muhimu katika maisha ya kila siku ya mwanafunzi kwani huakisi tabia njema kama nidhamu, uaminifu, heshima, na bidii kwa mwanafunzi mwenye ndoto ya kufanikiwa maishani, maadili haya huwa nguzo kuu inayomsaidia kufikia malengo yake.

Na Hagai Ruyagila

Wanafunzi wanaotarajia kuhitimu kidato cha sita katika Shule ya Sekondari Kasulu Mkoani Kigoma wametakiwa kuzingatia maadili mema, kuwaheshimu wazazi wao na kujiepusha na vitendo vya uhalifu ili kulinda mustakabali wao na kuwa raia wema katika jamii.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Kasulu Twalib Mangu wakati wa mahafali ya 16 ya kidato cha sita ambayo yamefanyika shuleni Hapo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Kasulu Twalib Mangu, Picha na Hagai Ruyagila

Amesema ni muhimu kwa wahitimu hao kutambua thamani ya elimu waliyoipata na kuitumia kwa manufaa yao binafsi na ya jamii kwa ujumla, huku akiwataka kuwa mabalozi wazuri wa nidhamu na maadili mema.

Sauti ya Mwenyekiti wa Bodi ya Shule

Mkuu wa Shule ya sekondari Kasulu Mwl Denis Kiloti amesisitiza umuhimu wa wanafunzi kuwaheshimu na kuwatii wazazi wao, huku akiwataka wazazi kuendelea kutimiza wajibu wao wa kulea, kuwasimamia na kuwaongoza watoto katika misingi bora ya maadili.

Sauti ya Mkuu wa Shule ya Sekondari Kasulu
Mkuu wa Shule ya sekondari Kasulu Mwl Denis Kiloti, Picha na Hagai Ruyagila

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi wilaya Ya Kasulu Mapigano nduhilubusa amesiwasisitiza vijana hao wanaotarajia kuhitimu kidato cha Sita kuepuka matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii.

Sauti ya Katibu wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Kasulu.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi wilaya Ya Kasulu Mapigano nduhilubusa, Picha Hagai Ruyagila

Baadhi ya wanafunzi wameeleza kufurahishwa na hatua waliyofikia huku wakiahidi kuwa waadilifu, kuitumia vyema elimu waliyoipata pamoja na kuzingatia maadili mema katika maisha yao yasasa baadaye.

Sauti ya wanafunzi