Joy FM
Joy FM
9 June 2026, 11:45

Viongozi wa dini wana nafasi kubwa katika kuiongoza jamii kiroho, kimaadili na kijamii. Kupitia mafundisho yao, viongozi hawa hutoa mwongozo unaowasaidia waumini kuishi kwa amani, upendo na mshikamano. Hivyo, ni muhimu viongozi wa dini kumtegemea Mungu na kuwa dira sahihi ya imani badala ya kuwa chanzo cha migogoro miongoni mwa waumini
Na Orida Sayon
Viongozi wa Kiroho (Dini ) Mkoani kigoma wamehimizwa kumtegemea mungu na kuwa dira sahihi ya imani badala ya
kuwa chanzo cha migogoro kwa waumini katika nyumba zao za ibada.
Hayo yamehimizwa na Mchungaji Charles Nkya wa Kanisa la PEFA kutoka Arusha wakati akitoa salamu za neno katika mahafali ya wachungaji ngazi ya stashahada katika chuo cha biblia cha Lake Tanganyika Christian College Manispaa ya
kigoma Ujiji.

Mchungaji Nkya amesema viongozi wa kiroho wanapaswa kua dira ya kuongoza waumini kufikia kusudi la Mungu wakijua
wana nafasi ya kuishawishi jamii kulinda amani na utulivu katika Nyanja mbalimbali katika jamii.
Wakisoma risala kwa Mgeni Rasmi, wahitimu wa masomo ya biblia chuoni hapo wameomba kuanzishwa kwa somo la saikolojia ngazi ya stashada na hapa baadhi yao wanaeleza namna somo la uongozi na Saikolojia linavyoweza kuwasaidia
katika kuongoza na kuhudumia watu wanaokubwa na changamoto za afya ya akili.

Baadhi ya viongozi wa chuo hicho Nathan Rathimhusein kwa njia ya mahojiano anajibu maombi ya wahitimu ya kuanzishwa kwa
baadhi ya masomo likiwemo somo la saikolojia