Joy FM

Bilioni 5 kuboresha miundombinu ya maji Kigoma Ujiji

19 May 2026, 10:12

Muonekano wa mabomba ya maji Manispaa ya Kigoma Ujiji, Picha na Mtandao

Maji ni rasilimali muhimu katika maisha ya binadamu na maendeleo ya taifa lolote na binadamu hutegemea maji kwa matumizi ya nyumbani, kilimo, ufugaji, viwandani pamoja na shughuli nyingine za kiuchumi.

Na Sadiki Kibwana

Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Manispaa ya Kigoma Ujiji  KUWASA imesema itaendelea kuwekeza zaidi katika ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya maji hasa katika maeneo korofi ili kuhakikisha upatikanaji wa maji unakuwa wa uhakika kwa wananchi.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja Mamlaka ya Maji Safi na Mazingira Manispaa ya Kigoma Ujiji KUWASA Filipo Funga, wakati akizungumza na kipindi hiki ambapo amesema maboresho hayo yatajikita katika maeneo yote korofi huku shilingi bilioni 5 zikitarajiwa kutumika.

Sauti ya Mkurugenzi KUWASA

Aidha ameongeza kuwa uwekezaji katika miundombinu ya maji ni muhimu na wamepanga kila mwaka kuboresha maeneo yenye miundombinu chakavu ili upatikanaji wa maji uwe wa kutosha wakati wote.

Sauti ya Mkurugenzi KUWASA

Baadhi ya wananchi wamesema mpango huo ukikamilika utakuwa na manufaa makubwa Katika upatikanaji bora wa huduma ya maji.

Sauti ya wananchi

Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha huduma ya maji nchini kwa kujenga na kuboresha miundombinu ya maji safi na usafi wa mazingira, ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo muhimu kwa urahisi na uhakika.