Joy FM

Kigoma: Wananchi watakiwa kuacha shughuli karibu na hifadhi za barabara

21 July 2023, 12:02

Mkuu wa Mkoa Kigoma Thobias Angenye akitoa hotuba wakati wa kikao cha bodi ya Barabara Mkoa,Picha na Josephine Kiravu

Wananchi Mkoani Kigoma wametakiwa kuacha kufanya shughuli za kibinadamu katika ya hifadhi za barabara

Na, Josephine Kiravu

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali Mstaafu wa jeshi la zimamoto na uokoaji Thobias Andengenye amewataka wakazi wa Mkoani hapa kufuata sheria na kuacha kufanya shughuli za kibinadamu katika  maeneo ya hifadhi za barabara.

Andengenye ametoa maelekezo hayo wakati akifungua kikao cha bodi ya barabara kwa Mkoa wa Kigoma ambapo amewaelekeza pia wakuu wa wilaya kusimamia ipasavyo na kamwe wasiruhusu wajasiriamali kufanya shughuli zao kwenye hifadhi za barabara.

Wajumbe wa bodi ya Barabara Mkoa wa Kigoma wakiwa katika kikao cha bodi hiyo, Picha na Josephine Kiravu
Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye

Ameongeza kuwa kuendelea kuwaacha wananchi kuishi na kufanya shughuli mbalimbali kwenye hifadhi za barabara kunachangia kusababisha fidia na madai yasiyokuwa ya lazima kwa Serikali pale wanapotakiwa kupisha maeneo hayo.

Kwa upande wake Meneja wa TANROADS mkoa wa Kigoma Mhandisi Narcis Choma amesema tatizo la uvamizi wa barabara sio kwa mjini pekee hata vijijini uvamizi wa barabara bado unaendelea kufanyika licha ya elimu inayoendelea kutolewa kwa jamii.

Sauti ya Meneja wa Tanroad Mkoa wa Kigoma

Katika hatua nyingine Mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini Kirumbe Ng’enda amezitaka Halmashauri Mkoani hapa kutenga bajeti kwa ajili ya ujenzi wa barabara kwenye fedha zinazotokana na mapato ya ndani ili kupunguza mzigo kwa TARURA.

Sauti ya Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini Kirembe Ngenda

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa ameitaka TANROADS na TARURA mkoani Kigoma kuongeza kasi kwenye ujenzi wa barabara pamoja na kuwachukulia hatua wakandarasi wazembe watakaoshindwa kukamilisha miradi kwa wakati ama kwenye ubora uliokusudiwa.

Baadhi ya wajumbe wa bodi ya Barabara Mkoa wa Kigoma wakiwa katika kikao cha bodi hiyo, Picha na Josephine Kiravu