Joy FM

Jeshi la polisi limekamata siraha mbili zilizotelekezwa buhigwe

21 February 2024, 16:28

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma, SACP, Filmon Makungu akionyesha vitu vilivyokamatwa katika oparesheni zinazoendelea Mkoani Kigoma, Picha na Lucas Hoha

Watu wasiojulikana wametelekeza siraha mbili katika kijiji cha Kibuye Wilayani Buhigwe Mkoani Kigoma

Na, Lucas Hoha

Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma limefanikiwa kukamata vitu mbalimbali ikiwemo silaha AK47 moja ikiwa na Magazine yenye risasi 22 na Chinese Pisto moja ikiwa na Magazine yenye risasi 7 zikiwa zimetelekezwa na watu wasiojulikana katika kijiji cha kibuye Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma.

Siraha zilizokamatwa na Polisi Kigoma, Picha na Lucas Hoha.

Hayo yamebainishwa na Kamanda wa polisi Mkoani Kigoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP Filemon Makungu wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya misako na operesheni mbalimbali zinazoendelea katika Wilaya zote za Mkoa wa Kigoma.

Sauti ya Kamanda wa jeshi la Polisi Kigoma, SACP Filmon Makungu

Aidha SACP Makungu amesema kwa upande wa kesi zilizopelekwa  Mahakamani washitakiwa watatu  wa kesi za kubaka wamehukumiwa vifungo tofautitofauti baada ya mahakama kuridhika na ushahidi wa upande wa jamhuri na kuwatia hatiani kwa kosa hilo, akiwemo Baraka Michael miaka 25 mkulima na mkazi wa Rutale ambaye amehukumiwa na Mahakama ya wilaya ya Kigoma kifungo cha kwenda jela miaka 30.

Sauti ya Kamanda wa jeshi la Polisi Kigoma, SACP Filmon Makungu

Wakati huohuo Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma linaendelea kuwaomba wananchi wa Mkoa huu kuendelea kushirikiana na jeshi la Polisi katika kuzuia na kubaini uhalifu na wahalifu kwa lengo lakuimarisha usalama wa raia na mali zao.