Joy FM

wapiga ramli chonganishi kuchukuliwa hatua kali za kisheria

28 March 2024, 11:55

Baraza la Madiwani katika halmashauri ya wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma limeazimia kuchukua hatua kali za kisheria kwa wapiga ramli chonganishi maarufu kamchape kufuatia kufanya shughuli za uvunjifu wa amani ndani ya halmashauri hiyo.

Kaimu Mkurugenzi akiwa amesimama na kulia kwake mwenyekiti wa halmashauri kushoto kwake ni katibu tawala wa wilaya ya Kasulu

Na, hagai Ruyagila

Katika kikao hicho cha baraza la madiwani cha robo ya pili ya mwaka 2023/2024 diwani wa kata ya bugaga Hitra Mlombero ameibua hoja ya kutaka kudhibiti kamchape na kuliomba jeshi la polisi kufanya operation maalumu ya kuhakikisha watu hao wanakamatwa.

Kufuatia kuibuka hoja hiyo mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kasulu Elia Kagoma ambaye pia ni diwani wa kata ya Kitanga amewaongoza wenzake kutaka kujua msimamo wa baraza hilo kuhusiana na suala la kamchape.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kasulu Emmanuel Ladislaus amesema halmashauri iko tayari kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuisaidia jamii na kuhakikisha wananchi wanakuwa salama na mali zao ili waweze kuendela na shughuli za uzalishaji mali pasipo kuwa na hofu yoyote.

Naye katibu tawala wilaya ya Kasulu Bi, Theresia Mtewele akimuwakilisha mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanal Isaac Mwakisu amesema amesuala hilo limeanza kuwa changamoto kwa jamii na sasa limeingia kwa viongozi hivyo amemuagiza mwenyeikiti wa halmashauri hiyo kutoa ushauri kwa serikali namna gani linaweza kutatuliwa