Joy FM

Waziri Pro. Mbarawa ashusha kibano kwa TRC

11 October 2023, 11:30

Waziri wa Ujenzi Pro. Makame Mbarawa akiwa katika ziara Mkoani Kigoma , Picha na Tryphone Odace

Katika kuhakikisha usafiri kwa kutumia treni unaimarika Waziri wa Uchukuzi Makame Mbarawa ameagiza watumishi wa Reli kufanya kazi kwa weledi na kujituma ili kuhaikisha wanatoa huduma bora.

Na, Tryphone Odace

Waziri wa  Ujenzi Pro. Makame Mbarawa ameonyesha kutoridhishwa utendaji wa kazi wa watumishi wa  Shirika la Reli Nchini TRC kwa kushindwa kusimamia na kutoa huduma bora kwa wateja.

Profesa Mbarawa ametoa kauli hiyo mara baada ya kutembelea ofisi ya reli Kigoma na Kukagua mabaehewa ya kubeba mizigo ambapo amesema utendaji kazi mzuri wa reli unategemea ufanisi mzuri wa watumishi walio tayari kufanya kazi.

‘Ni vyema wae ambao wanaona hawawez kufanya kazi watupishe kuliko  kuendelea kuharibu taswira ya shirika kwani Serikali imeendelea kuweka pesa ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora zaidi’

Aidha Pro. Mbarawa ameagiza uongozi wa reli kupunguza muda wa treni kuleta mizigo kwani wanatumia muda mrefu wa takribani wiki mbili kutoka Tanga hadi kufika Kigoma na kuchelewesha huduma kwa wananchi.

Waziri Mbarawa akinena jambo mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa shughuli za TRC, Picha na Tryphone Odace.

’Unakuta treni ya Simenti inatoka Tanga kuja Kigoma njiani inatumia wiki mbali na bado ikifika inachelewa kupakua hali hii haiwezi kuleta manufaa kwa Shirika na Serikali kwa ujumla na hivyo kaeni muone namna ya kupunguza muda angalau hata siku tano hivi anasema Mbarawa’

Naye Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa Shirika la Reli Bw. Senzi Kisengi amesema licha changamoto zinazowakabili hususani njia ya reli kutoka Kigoma hadi Tabora kuwa mbovu na treni kutembea polepole njiani lakini wataendelea kuboresha ili kuhakikisha wanakidhi mahitaji kwa wateja.

Kwa upande wao baadhi ya wafanyabiashara na wananchi wa Mkoa wa Kigoma wamesema ucheleweshaji wa mabehewa kupakua na kupakia mizigo imekuwa ikisababisha kukosa huduma zenye ubora na wengi wao kuingia gharama kubwa za uendeshaji wa biashara zao.