Joy FM

Rwizile: Haki za mtoto hazigawanyiki

11 March 2024, 16:47

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Kigoma Mhe. Augustine Rwizile amesema kila mtu ana haki ya kulinda na kuthamini haki za mtoto kwani haki hizi hazigawanyiki.

Na, Mwandishi wetu Winfrida Ngassa.

Mh Augustine Rwizile amesema hayo wakati afungua mafunzo kwa wadau walio mstari wa mbele katika kushughulikia mashauri ya watoto, na kuwa lengo ni kuhakikisha wadau wanaendelea kuelewa umuhimu wa haki za watoto mara tu wanapofikishwa mahakamani kama anavyoeleza.

Kwa upande wake, Afsa Ulinzi na Usalama wa Mtoto kutoka shirika la kuwahudumia watoto UNICEF Mkoa wa Kigoma Enna Lutengano amesema ukatili kwa watoto bado upo licha ya kuwa serikali inapambana katika kuhakikisha inadhibiti kesi hizi za ukatili kwa watoto.

Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo akiwemo afisa ustawi wa jamii Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Saada Aman wamesema mafunzo hayo yana tija kubwa katika kuhakikisha wanapambana na vita dhidi ya ukatili wa kijinsia kwa watoto.