Joy FM
Joy FM
20 June 2026, 13:15

Tamasha la Urithi wa Kihistoria na Utamaduni la Mji Mkongwe wa Ujiji lina umuhimu mkubwa katika kuhifadhi na kuendeleza historia, tamaduni na maadili ya jamii
Na Lucas Hoha
Tamasha la urithi wa kihistoria na utamaduni katika mji mkongwe wa Ujiji linatarajia kufanyika kuanzia tatehe 20 hadi 21 katika Manispaa ya Kigoma Ujiji likilenga kuwafindisha vijana kuwa na madili mema na kutangaza vivutio vya utali na wananchi kutambua fursa zilizopo katika mji huo wa ujiji na namna ya kuzitumia ili kujikwamua kiuchumi.
Hayo yamesemwa na Hamis Habiba Mkuu wa idara ya historia na malikale kutoka Ujiji Development and Heritage iliyoanzishwa mwaka 2024 katika Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Akizungumza na waandishi wa habari Bw. Hamis amesema kuna kila sababu za wananchi wa Mkoa wa Kigoma kutambua historia ya mji mkongwe wa ujiji ili waweze kuishi kwa kuzingatia maadili mama, kutunza amani na kufanya kazi kwa bidii.
Aidha Bw. Hamis amesema wananchi wa Mkoa wa Kigoma hususani wazazi na walimu ambao ni wazaliwa wa Kigoma kuwafindisha vijana ustaarabu wa watu wa kale wa ujiji ili waweze kuachana na masuala matumizi ya dawa za kulevya na kujikita katika shughuli za uzalishaji mali kwa kutambua historia yao.
Kwa upande wake, Idd Rajab ambaye ni mjumbe wa idara ya historia ya malikale kutoka Ujiji Development and Heritage amesema katika tamasha wamewaalika watu mbalimbali wa Mkoa wa Kigoma ili waweze kuwasilisha jumbe mbalimbali za kuonyesha urithi wa Mji wa Ujiji.