Joy FM
Joy FM
21 May 2026, 08:44

Mabadiliko ya tabianchi ni changamoto kubwa inayokabili dunia kwa sasa na athari zake zimeonekana kupitia ongezeko la ukame, uharibifu wa mazingira, kupungua kwa misitu na kuharibika kwa ardhi
Na Emmanuel Kamangu
Serikali kupitia mfuko wa dunia wa mabadiliko ya tabianchi (GCF) wameanza hatua za awali za kupanda miti na kuhamasisha kilimo mseto katika maeneo ambayo yameathiriwa na uwepo wa wakimbizi ili kuwajengea uwezo wananchi kuhimili mabadiliko ya tabia nchi katika maeneo hayo.
Akizungumza katika warsha hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanal Isack Mwakisu katika kikao kazi hicho amacho kimelenga kuthibitisha vigezo vya kuchagua maeneo kwa ajili ya usimamizi shirikishi wa mistu ya jamii , kupanda miti na kilimo mistu amewahakikishia usalama na ushirikiano wa kutosha Tasisi ya utafiti wa misitu Tanzania (TAFORI) ambao ndio watoa ushauri wa kiufundi wa mradi sambamba na ofisi ya makamu wa raisi mazingra ili kuhakikisha mradi huo unafanikiwa ipasavyo kwa manufa ya wananchi.

Mtafiti kutoka Taasisi ya utafiti Tanzania Dkt. Numan Amanzi pamoja Afisa Mazingira Mwandamizi kutoka Ofisi ya makamu wa Rais Bw. Isack Emmanuel wamesema katika mradi huo wanakusudia kuwajengea uhimilivu wananchi wa wilaya za Kasulu, kakonko na Kibondo juu ya athari za mabadiliko ya tabianchi ambayo yametokana na uwepo wa shuguli za wakimbizi.

Kwa upande wao, Wataalamu wa idara mbali mbali kutoka katika wilaya hizo ambao wameshiriki kikao kazi hicho mmoja wao akiwa Bi. Dorisia kashoa wamesema mradi huo ambao umelenga kuwajengea uwezo wananchi juu ya namuna ya kukabiliana na mabadiiko ya tabia nchi utasaidia sana kuondokana na maeneo mengi kuwa jangwa na kurejesha uoto wa asili.
