Joy FM
Joy FM
11 November 2024, 17:03

Halmshauri ya wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma imepokea jumla ya mapingamizi 25 kutoka vyama vya siasa vitakavyoshiriki uchaguzi wa serikali za mitaa wilayani humo.
Na Emmanuel Kamangu – Buhigwe
Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma Bw, George Emmanuel mbilinyi amesema zoezi la kuchukua na kurejesha fomu za uchaguzi wa serikali za mitaa wilayani humo limefanyika kikamilifu kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na Serikali.
Bw, Mbilinyi amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Wilayani Buhugwe ambapo ameeleza kuwa baadhi ya taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kufungwa kwa ofisi na wagombea kushindwa kuwasilisha mapingamizi siasahihi kwani zoezi limefanyika vizuri na kwa ukamilifu.
Aidha Bw, Mbilinyi amevitaka vyama vya siasa kufanya kampeni za kistaarabu wakati utakapowadia ili kuepuka kuzua taharuki kwa Wananchi.
Hata hivyo Bw. Mbilinyi Ameongezea kuwa kwa Wilaya ya Buhigwe kuna jumla ya mapingamizi 25 ambayo yamewasilishwa kutoka vyama sita vya siasa ambavyo ni Chadema, NCCR Mageuzi, CUF, Act Wazalendo na CCK.