Joy FM

Walimu watakiwa kufundisha kwa bidii ili kuinua ufaulu

9 July 2024, 14:26

Afisa mtendaji wa kata ya Murusi Ndugu Omary Sebabili, Picha na Hagai Ruyagila

Serikali imesema itaendelea kutatua na kushughulikia changamoto za walimu ili waweze kufanya kazi bila vikwazo vinavyowakabili.

Na Hagai Ruyagila – Kasulu

Waalimu wa Kata ya Murusi Halmashauri ya Mji Kasulu Mkoani Kigoma wametakiwa kusimamia nidhamu bora kwa wanafunzi wao ili kuinua sekta ya elimu ndani ya kata hiyo.

Rai hiyo imetolewa na Afisa mtendaji wa kata ya Murusi Ndugu Omary Sebabili wakati akizungumza katika kikao na waalimu wa shule za msingi na sekondari ndani ya ukumbi wa mikutano wa shule ya sekondari Bogwe.

Amesema nidhamu inasaidia kwa kiasi kikubwa kufikia mafanikio katika sekta ya elimu ambayo imekuwa ikipanda kwa kasi kubwa katika kata ya Murusi.

Sauti ya Afisa mtendaji wa kata ya Murusi Ndugu Omary Sebabili

Kwa upande wake afisa elimu kata ya Murusi Gervas Mgeze amesema changamoto ya nidhamu kwa kiasi kikubwa ipo kwa wanafunzi na wanaendelea kuifanyia kazi lakini kwa upande wa waalimu inaridhisha.

Sauti ya afisa elimu kata ya Murusi Gervas Mgeze

Nao baadhi ya waalimu walioshiriki katika kikao hicho wamesema mwalimu ni mzazi na anatakiwa kusimamia nidhamu ya mwanafunzi ili kumuandaa mtoto kuwa kiongozi bora katika jamii inayomzunguka.

Sauti ya waalimu walioshiriki katika kikao hicho