Joy FM

Madereva wanaokiuka sheria za barabarani kufutiwa leseni

8 August 2024, 09:56

Waendesha pikipiki maarufu bodaboda wakiwa katika kijiwe wakisubiri abiria, Picha na Mtandao

Mkuu wa wilaya buhigwe Michael Ngayalina amelitaka jeshila Polisi wilayano humo kuwachukulia hatua za kisheriamadereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali.

Na Michael Mpunije – Buhigwe

Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani wilayani Buhigwe Mkoani Kigoma Limetakiwa kusimamia sheria za usalama barabarani kwa kuwatoza faini waendesha vyombo vya moto kulingana na kosa wanapobainika kukiuka sheria za usalama Barabarani.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa wilaya ya Buhigwe kanali Michael Ngayalina wakati akijibu malalamiko ya wananchi wa kijiji cha Songambele wilayani humo.

Kanali Ngayalina amesema watashughulikia malalamiko ya wananachi na kuhakikisha sheria za usalama barabarani zinazingatiwa ili kupunguza ajari za barabarani zinazotokana na uzembe wa madereva. 

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Buhigwe kanali Michael Ngayalina

Aidha ameongeza kwa kuwataka waendesha vyombo vya moto wilayani Buhigwe kufuata sheria za Usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kuheshimu vizuizi vinavyowekwa  katika maeneo ambayo ujenzi wa barabara unaendelea.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Buhigwe kanali Michael Ngayalina

Kwa upande wao baadhi ya waendesha pikipiki maarufu Bodaboda wilayani Buhigwe wameliomba jeshi la polisi kuendelea kufuatilia baadhi ya madereva wanaokiuka sheria ili waweze kuchukuliwa hatua kwa lengo la  kupungunza ajari barabarani.