Joy FM

DC Kasulu aeleza kutoridhishwa na ufaulu  wa wanafunzi matokeo ya darasa la 7

12 December 2024, 09:21

Mkuu wa Wilaya Kasulu Kanali Isac Mwakisu, Picha na Michael Mpunije

Idara ya elimu Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma imetakiwa kuanza kufuatilia walimu ambao hawawajibiki ipasavyo katika suala la ufundishaji hali inayosababisha matokeo kuendelea kuporomoka katika wilaya hiyo hasa katika matokeo ya darasa la saba.

Na Michael Mpunije – Kasulu

Mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali Isaac mwakisu ameeleza kutoridhishwa na mwenendo wa ufaulu  wa wanafunzi kwenye matokeo ya darasa la 7 atika shule za msingi zilizopo katika halmashauri ya mji Kasulu baada ya halmshauri hiyo kushika nafasi ya 6 kimkoa kati ya halmashauri 8 za mkoa wa Kigoma

Katika kikao cha baraza la madiwani la halmshauri ya mji Kasulu mkuu wa wilaya ya Kasulu kanali Isaac mwakisu ametoa maagizo kwa mkurugenzi na afisa elimu wa halmashauri hiyo kuhakikisha wanafuatilia na kubaini sababu za kiwango Elimu kushuka katika matokeo ya darasa la 7 katika halmshauri hiyo.

Kanali mwakisu amesema anataka kuona kiwango cha ufaulu kinapanda ili kushika nafasi nzuri kimkoa kwa shule za msingi za Serikali na kuitaka idara ya elimu kuwasilisha changamoto zinazowakabili ziweze kutatuliwa.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali Isaac mwakisu

Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa halmshauri ya mji kasulu bw.Selemani kwirusha ameeleza kusikitishwa na matokeo ya darasa la 7 na kuwataka madiwani kushirikiana katika kukuza taaluma ya wanafunzi shuleni ambapo halmashauri ya mji kasulu imeshuka mpaka nafasi ya 6 kutoka nafasi ya 4 kimkoa mwaka uliopita kati ya halmashauri 8 za mkoa wa Kigoma kushuka katika.

Sauti ya Bw.Selemani kwirusha

Mkurugenzi wa halmshauri ya mji kasulu Mwl vumilia Simbeye amesema wameshaanza ufuatiliaji na kutoa maagizo wakuu wa shule za msingi kuhakikisha wanasimamia waalimu ili waweze kufanya jitihada za kukuza taaluma ya wanafunzi shuleni.

Sauti ya Mkurugenzi Mwl vumilia Simbeye

..