Joy FM

Akutwa amefariki, mwili ukiwa kwenye kiroba Buhigwe

17 April 2026, 1:05 pm

Picha ya mfano wamtu aliyeuwawa na kutupwa kwenye kiroba, Picha na Mtandao

Serikali inapaswa kuhakikisha sheria dhidi ya mauaji zinatekelezwa kikamilifu, na wahusika wanachukuliwa hatua haraka.

Na Michael Mpunije

Mwanaume mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 30-35 ambaye hajatambulika uraia wala kabila lake amekutwa akiwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa umefungwa kwenye kiroba na kutelekezwa kando ya Barabara katika Kijiji cha Kimara kata ya Kinazi wilayani Buhigwe Mkoani Kigoma.

Tukio hilo limetokea April 16,2026 baada ya wasamalia wema wakiwa katika shughuli zao kubaini hali isiyo ya kawaida ya kiroba hicho kikiwa kimetelekezwa kando ya Barabara na kutoa taarifa katika uongozi wa Kijiji ili kuwasiliana na mamlaka husika kwa ajili ya kufanya uchunguzi.

Akizungumza kwa njia ya Simu mwenyekiti wa Kijiji cha Kimara kata ya Kinazi Bw.Medadi Jeremiah ameeleza kusikitishwa na tukio hilo na kusema kuwa baada ya kufanyika kwa uchunguzi wa jeshi la Polisi na kuthibitisha kuwa mwanaume huyo alikuwa tayari ameshafariki waliruhusu mwili huo kufanyiwa mazishi.

Sauti ya Mwenyekiti Kimara

Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha kimara wameliomba jeshi la Polisi kufanya uchunguzi na kubaini waliohusika na tukio hilo huku wakitoa rai kwa jamii Kuwa na upendo kwa kuzingatia maadili mema ili kudumisha amani