Joy FM

Vibanda 9 vya biashara vyateketea kwa moto Kigoma

23 May 2026, 13:23

Baadhi ya wafanyabiashara wakiwa katika eneo ambalo vibanda vimeteketea kwa moto, Picha na Tryphone Odace

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro amekagua kisha kuzungumza na wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao katika soko la Kibirizi, Manispaa ya Kigoma Ujiji, kufuatia kuungua kwa baadhi ya vibanda vya biashara visivyo vya kudumu, vilivyojengwa jirani na soko hilo.

Na Tryphone Odace

Mkuu wa Mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro ameagiza kufanyika kwa uchunguzi na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa yeyote aliyehusika na tukio la moto uliosababisha jumla ya vibanda tisa vya biashara kuteketea kwa moto katika soko la Kibirizi Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Muonekano wa eneola vibanda vya biashara vilivyoteketea kwa moto eneo la Kibirizi Manispaa ya Kigoma, Picha na Tryphone Odace

Akizungumza na wafanyabiashara baada ya kutembelea eneo hilo, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Balozi Simon Sirro  ameagiza uchunguzi wa kina kufanyika mara moja ili kubaini aliyehusika  aweze kuchukuliwa hatua na kuwaomba wafanyabiashara kuendelea na shughuli zao wakati wakisubiri sokola jipya la Kibirizi likamilike ili waweze kuhamia katika soko hilo.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro

Awali akitoa taarifa ya tukio hilo mbele ya Mkuu wa Mkoa Kigoma, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kigoma Michael Maganga amesema uchunguzi wa awali unaonesha kuwa chanzo cha moto huo jiko la mkaa liliachwa na mmoja wa wafanyabiashara akiwa ameinjika maharage katika eneo hilo.

Sauti ya Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kigoma Michael Maganga
Muonekano wa eneola vibanda vya biashara vilivyoteketea kwa moto eneo la Kibirizi Manispaa ya Kigoma, Picha na Tryphone Odace

Baadhi ya wafanyabiashara waliozungumza na Joy Fm wameiomba serikali kuwasaidia mikopo wafanyabiashara walioathirika na tukio hilo la moto ili waweze kurejea katika shughuli zao za kila siku.

Sauti ya Wafanyabiashara

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa Kigoma, Balozi Simon Sirro ameelekeza wananchi kuendelea kushirikiana katika suala la ulinzi wa maeneo ya biashara ili kukabiliana na watu wenye nia ovu katika maeneo yao