Joy FM

Serikali yakabidhi mlima Sunzu kwa TFS Kasulu

18 June 2026, 20:15

Baadhi ya wananchi wakiwa katika mkutano wa serikali ikikabidhi Mlima Sunzu kwa TFS, Picha na Sadick Kibwana

Mlima Sunzu umekabidhiwa kwa Wakala wa Misitu Tanzania TFS huku baadhi ya wananchi wakieleza kutoridhishwa na uamzi huo

Na Sadick Kibwana

Halmashauri ya Mji wa Kasulu Mkoani Kigoma imekabidhi umiliki wa Mlima Sunzu kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), kwa ajili ya uendelezaji wa shughuli mbalimbali na usimamizi kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wananchi uliofanyika katika Mtaa wa Sunzu Kata ya Kumnyika Wilayani humo, Kaimu Mkurugenzi Mji Kasulu ambaye ni Mganga Mkuu Wa Halmashauri hiyo Dkt. Nangi William Nangi, amesema uamuzi huo umetokana na umuhimu mkubwa wa eneo hilo la kimkakati.

Baadhi ya viongozi wakiwa katika mkutano wa serikali kukabidhi Mlima Sunzu kwa TFS, Picha na Sadick Kibwana

Aidha, Ofisa Ardhi wa Halmashauri ya Mji Kasulu, Bw. Pesha Jackson, amewasihi wananchi wenye malalamiko au madai kuhusu eneo hilo kufika ofisini kwake ili kupata ufafanuzi wa kina wa kisheria.

Naye Mwanasheria wa Halmashauri hiyo, Edwin Rwekaza, amebainisha kuwa taratibu zote za kisheria zitazingatiwa na kuwataka wananchi wenye malalamiko kuyapeleka ofisini kwake kwa ajili ya utatuzi.

Pamoja na uamuzi huo, baadhi ya wananchi wameibua hisia na maoni tofauti kuhusu hatua hiyo ya makabidhiano.

Mkutano huo umeshuhudiwa na wananchi kutoka kata zinazozunguka mlima huo, ikiwemo Nyansha, Muhunga, na Kumnyika, ambapo eneo hilo la mlima limekabidhiwa rasmi chini ya ulinzi wa TFS.