Joy FM
Joy FM
30 April 2026, 11:40

Baraza la madiwani katika Manispaa ya Kigoma Ujiji limeketi kwa ajili ya kupokea taarifa za Kata na baraza hilo limehudhuriwa na kamati ya Ulinzi na Usalama, viongozi wa vyama vya siasa, wakuu wa Idara na vitengo, watendaji wa Kata, waandishi habari pamoja na Wananchi.
Na Mwandishi wetu
Madiwani katika Manispaa ya Kigoma Ujiji, Mkoani Kigoma wameiomba serikali kuwa na utaratibu wa kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi kwa wakati kutokana na mvua nyingi kunyesha, kufuatia uharibifu wa miundombinu ya barabra na taasisi za elimu.
âWakizungumza wakati wa kikao cha baraza la madiwani cha uwasilishaji wa taarifa za kata madiwani hao wamesema changamoto hizo zinapokosa ufumbuzi zinasababisha wananchi kukosa huduma za kijamii kwa wakati.

Kwa upande wake Mtahiki Meya Manispaa ya Kigoma Ujiji Musa Maulid amesema, kutokana na adha za taasisi za Elimu kuvamiwa na maji na miundombinu kuharibika, wanalazimika kufanya ziara kuchunguza kwa kina ili kuchukua hatua za kutatua kero hizo.
