Joy FM

Kigoma kuwa lango la uchumi kwa nchi za Afrika Mashariki

16 April 2026, 9:38 am

Baadhi ya wafanyabiashara na viongozi mbalimbali wakiwa katika mkutano wa kongamano la biashara mjini Kigoma, Picha na Lucas Hoha

Fursa nyingi za kiuchumi ambazo bado hazijatumika kikamilifu na kuleta tija ya kiuchumi kwa wananachi na taifa kwa ujumla zimeelzwa kuwepo katika Mkoa wa Kigoma

Na Lucas Hoha

Naibu waziri wa Viwanda na Biashara nchini Tanzania David Londo amewahakikisha wawekezaji kutoka jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa serikali imeufungua Mkoa wa Kigoma kuwa wa Kibiashara na kuwataka wawekezaji kujitokeza kuwekeza ili kukuza uchumi kwa maendeleo ya nchi za Afrika Mashariki.

Naibu waziri wa biashara Mh. Londo ameyasema hayo wakati akifungua Kongamano la Biashara na uwekezaji la Ziwa Tanganyika ambalo limefanyika mjini Kigoma

Amesema uwepo wa Ziwa Tanganyika ambalo linaunganisha nchi zaidi ya tatu 3 ikiwemo Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ni mlango muhimu utakaowezesha biashara kufanyika kwa ufanisi.

Sauti ya Naibu waziri wa Viwanda na Biashara nchini Tanzania David Londo

Awali Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro ametaja baadhi ya miradi ya kimkakati ambayo imetekelezwa na serikali katika ikiwemo kupatikana na umeme wa uhakika, ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami na uboreshaji wa Meli ya Mv. Liemba  ambao umefikia zaidi ya asilimia 50.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro

Kwa upande wao baadhi ya wafanyabiashara wa Mkoa wa Kigoma wamesema serikali kuufungua mkoa wa kigoma ni suala muhimu, huku wakiomba kuwepo kwa ushirikiano baina ya nchi zinazozunguka ziwa Tanganyika ili kuboresha usafiri na usafirishaji wa bidhaa na abiria katika Ziwa hilo.

Sauti ya baadhi ya wafanyabiashara wa Mkoa wa Kigoma

Kongamano hili linaonesha taswira madhubuti ya jitihada za serikali za kuifanya Kigoma kama eneo la kimkakati kw kuwa kitovu cha biashara kwa biashara za mpakani kwa nchi zinazozunguka Ziwa Tanganyika kama Burundi, Rwanda, Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo