Joy FM
Joy FM
14 Aprili 2026, 13:14

Kuhifadhi chakula kwenye vyombo vya plastiki ni jambo la kawaida, lakini linaweza kuwa na madhara fulani kiafya na kwa ubora wa chakula hasa kama plastiki si salama au ikitumika vibaya.
Na Emmanuel Kamangu
Wanaotumia vyombo vya plastiki kuhifadhia vyakula vya moto wako harini kukumbana na saratani ya tumbo sambamba na saratani ya koo.
Matumizi ya vyombo vya plastiki hasa kwa mama ntilile au katika baadhi ya migahawa kumetajwa kuwa ni jambo linalokinzana na kanuni za kiafya kutokana na madhara yatokanayo na kutoa huduma ya chakula kwa mteja katika sahani za plastiki hasa chakula cha moto.
Gribeti Mosh ni Mratibu wa huduma za shirika la Viwango Tanzania TBS katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu hapa anafafanua kwa undani jinsi ilivyohatari kiafya kutumia chakula cha moto katika sahani za plastikini kutokana na vyombo hivyo kuwa vitu vinavyoitwa micro plastiki ambavyo ni hatari kwa afya ya mwanadamu.
Aidha Bw, Mosh ameendelea kuwasihi wanaotoa huduma ya chakula katika migahawa na wachoma chips kuacha kufungia wateja wao chakula katika mifuko ya Naironi kwani kufanya hivyo ni kuhatarisha afya ya mraji.
Kwa upande mwingine Bw, Mosh amewataka wanaotoa huduma za chakula katika maeneo mbali mbali ya mji wa kasulu kuhakikisha wanatumia aluminium foil paper kufungia mteja vyakula vya moto kwani ni salama tofauti na kutumia mifuko ya nairon.
Hata hivyo Bw, mosh amewasihi wananchi wanaopata chakula katika migahawa kukataa kuhudumiwa chakula katika sahani za plastiki jambo litakalosaidia kuendelea kukabiliana na wimbi hilo.