Joy FM

Wahitimu kidato cha sita waaswa kuwa wazalendo

20 April 2026, 09:11

Wahitimu wa kidato cha sita shule ya sekondari ujiji, Picha na Sadick Kibwana

Wakati wanafunzi wa kidato cha sita wakiwa wanajianda na mitihani ya kuhitimu elimu ya kidato cha sita wameaswa kusaoma kwa bidii ili waweze kufanya vizuri katika mitihani yao

Na Sadiki Kibwana

Wanafunzi wanaohitimu kidato cha sita Wilaya ya Kigoma wametakiwa kuwa wazalendo na kuepukana na makundi yasiyofaa ili kutimiza ndoto zao.

Hayo yamesemwa na Mh. Kirumbe Shaban Ng’enda Naibu Katibu Mkuu CCM Jumuiya ya Wazazi Tanzania bara katika mahafali ya 16 ya kidato cha 6 katika Shule ya Sekondari Ujiji High iliyopo wilayani humo mkoani Kigoma.

Kirumbe Shaban Ng’enda Naibu Katibu Mkuu CCM Jumuiya ya Wazazi Tanzania bara akiwa katika mahafali ya kidato cha sita Ujiji Sekondari

Amesema wanafunzi wanapaswa kuwa wazalendo na nchi yao pia amewaomba wadau wa elimu kushirikiana kwa pamoja kuendeleza elimu wilayani humo.

Aidha Mkuu wa shule hiyo Bi .Tirisa Sadock amesema shule hiyo imekuwa na changamoto nyingi ameomba wadau kuwasapoti.

Baadhi ya viongozi wakiwa katika mahafali ya kidato cha sita shule ya sekondari ujiji, Picha na Sadick Kibwana

Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi wa kidato cha sita shuleni hapo wamesema haikuwa rahisi lakini mungu kafanikisha hilo.

Mahafali hayo yamehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa chama, walimu pamoja na wazazi yakilenga kuwatia moyo kuendelea kufanya vizuri katika hatua inayofuata ya maisha yao.

Wahitimu wa kidato cha sita shule ya sekondari ujiji, Picha na Sadick Kibwana