Joy FM

Mwenyekiti wa madiwani aahidi uwajibikaji kwa chama na wananchi

15 August 2026, 12:18

Mwenyekiti wa madiwani Tanzania ambaye pia ni diwani wa Kata ya Kazuramimba akiwa amewasili Kigoma, Picha na Mwandishi wetu

Diwani wa Kata ya Kazuramimba Mh. Musa Chesa ambaye amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Madiwani Tanzania kupitia Chama cha ACT – Wazalendo amesema katika nafasi hiyo atahakikisha anashirikiana na viongozi wa chama na serikali katika utekelezaji wa majukumu ya kusukuma maendeleo ya wananchi mbele

Na Mwandishi wetu

Mwenyekiti wa Madiwani wa Chama cha ACT-Wazalendo Tanzania ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kazuramimba,Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma  Musa Chesa, ameahidi kuendelea kusimamia haki na uwajibikaji katika kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa wakati na kuwanufaisha wananchi.

Mwenyekiti wa madiwani Tanzania ambaye pia ni diwani wa Kata ya Kazuramimba akisalimiana na wanachama wakimpokea, Picha na Mwandishi wetu

Akizungumza na waandishi wa habari, mjini Kigoma, Chesa amesema atahakikisha anasimamia haki, ukweli na uwajibikaji katika nafasi yake ya udiwani na Mwenyekiti wa madiwani wa chama cha ACT – Wazalendo Tanzania, ili kila mwananchi apate haki yake na kunufaika na matokeo ya usimamizi bora wa miradi ya maendeleo.

Aidha amesema atatumia nafasi yake ya udiwani pamoja na uongozi wa madiwani wa ACT-Wazalendo kuhimiza ushirikiano, uwajibikaji na mawasiliano mazuri kati ya wananchi, Halmashauri na Serikali katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Mwenyekiti wa madiwani Tanzania ambaye pia ni diwani wa Kata ya Kazuramimba akisalimiana na wanachama wakimpokea, Picha na Mwandishi wetu

Ameutaja ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kazuramimba kuwa miongoni mwa miradi hiyo, akisema kituo hicho kinatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni na kitasaidia kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wa kata hiyo na maeneo jirani.

Kwa upande wao, baadhi ya viongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Mkoa wa Kigoma, akiwemo Mwenezi wa chama hicho, wamesema Mwenyekiti wa Madiwani wa ACT-Wazalendo Tanzania ana jukumu la kusimamia malengo ya chama kwa kuhakikisha anafika katika kata mbalimbali, kusikiliza changamoto za wananchi na kushirikiana nao katika kuzitafutia ufumbuzi.

Viongozi hao wameeleza kuwa ushirikiano kati ya viongozi, wananchi, Halmashauri na Serikali ni muhimu katika kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa ufanisi na inaleta matokeo yanayotarajiwa kwa jamii.

Mwenyekiti wa madiwani Tanzania ambaye pia ni diwani wa Kata ya Kazuramimba akisalimiana na wanachama wakimpokea, Picha na Mwandishi wetu