Joy FM

Wajasiriamali mwalo wa Kalalangabo Kigoma waomba barabara kuboreshwa

21 August 2026, 13:49

Baadhi ya wajasiriamali wakiwa katika mwalo wa Kallangabo, Picha na Josephine Kiravu

Uboreshaji wa miundombinu ni sehemu ya mkakati wa kukuza na kustawisha biashara za wajariamali na kuongeza kipato cha familia zao na Taifa kwa ujumla

Na Josephine Kiravu

Wajasiriamali katika mwalo wa Kalalangabo kata ya Ziwani Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma wameiomba Serikali kuboresha miundombinu ya barabara kutoka eneo hilo kuelekea kibirizi sambamba na kusimamia vyema usafi wa mazingira mwaloni hapo.

Mwalo wa kalalangabo ni bandari ndogo ya uvuvi na eneo muhimu la mwambao lililoko katika Ziwa Tanganyika na eneo hili hutumika kwa shughuli za uvuvi na usafirishaji na kuvuka maji.

Hata hivyo licha ya kuwa na idadi kubwa ya wajasiriamali wanaotegemea eneo hilo lakini mazingira yake bado si rafiki kama wanavyoeleza akina mama hawa wanaotegemea mwalo huo kwa shughuli za biashara.

Sauti ya wajasiriamali

Na hapa wanaeleza namna wanavyoathiriwa na ubovu wa miundombinu ya barabara wanaoutumia kufika kibirizi.

Sauti ya Sauti ya wajasiriamali
Muonekano wa Mwalo wa Kalalangabo, Picha na Josephine Kiravu

Diwani wa kata ya Ziwani ambae pia ni makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kigoma amesema tayari ametoa maelekezo kwa uongozi wa kata kushughulikia wanaoharibu mazingira ya eneo hilo.

Sauti ya Diwani wa kata ya Ziwani

Hata hivyo kuhusu suala la miundombinu ya barabara amewataka wananchi kuwa wavumilivu kwani suala hilo tayari lipo Serikalini.

Sauti ya Diwani wa kata ya Ziwani
Muonekano wa dagaa za wajasiriamali wa mwalo wa Kalalangabo, Picha na Josephine Kiravu

Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 Kata ya Ziwani ina idadi ya watu wapatao 9,537 ambapo biashara kuu wanayotegemea ni mazao yatokanayo na uvuvi katika Ziwa Tanganyika.