Joy FM

Mwenge wa uhuru kuzinndua miradi ya bilioni 73.2 Kigoma

8 September 2026, 01:02

Mkuu wa Mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro akipokea mwenge wa uhuru baada ya kuwasili katika Wilaya ya Kakonko kutoka Wilayani Biharamulo Mkoani Kagera, Picha na Mwandishi wetu

Mwenge wa uhuru umewasili Mkoani Kigoma ambapo umepokelewa katika Halmashauri ya Wilaya Kakonko na unatarajia kutembelea, kukagua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo

Na Mwandishi wetu

Mwenge wa Uhuru umepokelewa na kuanzia mbio zake Mkoa wa Kigoma katika Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko, ambapo jumla ya miradi yenye thamani ya Shilingi Bil.73.2 itazinduliwa, kutembelea, kukaguliwa sambamba na kukabidhi Hundi, vifaa na Samani.

Mkuu wa Mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro akipokea mwenge wa uhuru baada ya kuwasili katika Wilaya ya Kakonko kutoka Wilayani Biharamulo Mkoani Kagera, Picha na Mwandishi wetu

Mwenge wa Uhuru utakimbizwa umbali wa Km. 937.8 katika Halmashauri Nane za Mkoa ambapo katika miradi itakayofikiwa, mchango wa Serikali na wahisani ni Shilingi. Bil.57.5, wahisani Bil.14.6, Halmashauri Mil. 958.4 huku nguvu ya wananchi ikiwa Mil.100.6.

Aidha, Miradi 20 itawekewa mawe ya msingi, 16 itazinduliwa, 12 itatembelewa na kukaguliwa  huku mingine minne itahusisha kukabidhi vifaa, Hundi au Samani.

Mkoani hapa, Mwenge utakimbizwa kuanzia leo Septemba 7 hadi 14, 2026 kisha kukabidhiwa katika Mkoa wa Tabora Septemba 15, 2026.