Joy FM
Joy FM
19 September 2026, 10:45

Usafi wa mazingira ni jambo muhimu katika maisha ya binadamu na mazingira safi humsaidia mtu kuishi katika hali nzuri na humkinga dhidi ya magonjwa mbalimbali
Na Lucas Hoha
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dkt. Rashird Chuachua amewaagiza Watendaji wa kata zilizopo Manispaa ya Kigoma Ujij kuwatoza faini wananchi wanaochafua Mazingira kwa kutupa taka ovyo ili kuhakikisha Manispaa ya Kigoma Ujiji na maeneo mengine ya Wilaya hiyo yanakuwa safi muda wote.

Chuachua ameyasema hayo wakati akikabidhi Pikipiki za miguu Mitatu maarufu kama Guta kwenye idara ya usafi wa Mazingira Katika Manispaa ya Kigoma Ujiji ambazo zinatafanya usafi kwa baadhi ya Kata za Manispaa hiyo ikiwemo Kata ya Mwanga Kaskazini na Kata ya Gungu
Amesema ili kukomesha tatizo la baadhi ya watu wanaochafua mazingira kwa makusudi sasa watendaji wa kata wataanza kukamata watu wa wanaochafua mazingira nakuwatoza faini pale inapobidi

Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Mussa Maulid pamoja n mambo mengine amewataka watendaji wa kata ambao wamepewa Maguta hayo kuhakikisha wanayatunza ili yafanye kazi ya usafi kwa muda mrefu
Awali Afisa Usafi wa Mazingira katika Manispaa ya Kigoma Ujiji Petronila Gwakila akitoa taarifa ya pikipiki za Miguu Mitatu amesema zimeghalimu zaidi ya shilingi Milioni 50 ambazo zimetengwa kutokana na mapato ya ndani lengo likiwa ni kurahisisha shughuli za usafi wa mazingira katika Manispaa hiyo
