Joy FM
Joy FM
10 September 2026, 13:21

Kukamilika kwa mradi wa maji Nyamnyusi utasaidia kupunguza changamoto za wananchi kutembea umbali mrefu kutafuta huduma ya maji
Na Emmanuel Kamangu
Mwenge wa uhuru 2026 umekagua na kuzindua mradi wa maji wenye thamani ya zaidi ya Bilion 1 katika kijiji cha nyamnyunsi halmashauri ya wilaya ya kasulu ikiwa ni mwendelezo wa mkakati wa serikali wa kuhakikisha inamtua mama ndo kichwani.
Akisoma taarifa za mradi huo meneja wakala wa maji na usafi wa mazingra vijijini Rwaasa Bw, Edward Kisalu amebainisha kuwa mradi unaenda kukabiliana na kero ya maji kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuondokana na kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya maji safi na salama.

Serikali kwa kushirikiana na wananchi wameendelea kuwa na umoja katika kuhakikisha shuguli mbali mbali za maendeleo zinakamilika kwa wakati na mradi huu wa maji kimsigi wananchi wamejitolea eneo la kujenga matenki haya mawili.
Akizungumza mara baada ya kuzindua mradi huo kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2026 Bw,Wazo Michael Mwang’onda amewahimiza wananchi wa kijiji cha Nyamnyunsi kuhakikisha wanapanda miti rafiki ya maji katika chanzo , kutokuchoma moto ovyo ikiwemo kutunza vizuri miundombinu ya maji jambo litakalo saidia kuwepo kwa maji ya uhakika.
Swala la kumtua mama ndoa kichwani ni mpango wa serikali katika kuboresha sekta ya maji nchini kwa lengo la kufanya wananchi wapate huduma ya maji karibu na makazi yao.
Kwa upande wao wananchi wa kijiji cha Nyamnyusi mmoja akiwa Bi Rozalia john wameishukuru serikali kwa kukamilika kwa mradi huo wa maji na kuwa itawasaidia kupata maji karibu tofauti na awali ambapo wamekuwa wakitembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo.
Hata hivyo wananchi hao wameongeza kuwa hapo awali wamekuwa wakiugua matundo,kuhara na kuugua ugonjwa kichocho kutokana na kutumia maji ambayo siyo salama na kupelekea kuwa na afya hafifu.