Joy FM

RC Kigoma aagiza mkandarasi kukamilisha mradi wa kituo cha forodha Buhigwe

10 July 2026, 11:07

Mkuu wa Mkoa Kigoma akiwa nabaadhi ya viongozi wakati alipotembelea miradi ikiwemo mradi wa kituo cha pamoja, Picha na , Mwandishi wetu

Utekelezaji wa mradi wa kituo cha pamoja cha forodha unatajwa kuchochea na kukuza uchumi wa wananchi wa pande zote mbili Tanzania na Burundi

Na Mwandishi wetu

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro amemuagiza Mkandarasi wa ujenzi wa mradi wa kituo cha Pamoja cha forodha kinachojengwa Wilayani Buhigwe kwa thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 47 kuongeza kasi ya ujenzi wa mradi huo ili uweze kukamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.

Balozi Sirro ametoa maagizo hayo julai 9,2026 wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo wilayani Buhigwe ambapo ameeleza kuwa mradi utakapokamilika utakuwa na manufaa makubwa kwa wananchi.

Mkuu wa Mkoa Kigoma akizungmza wakati alipotembelea mradi wa kituo cha pamoja cha forodha Buhigwe, Picha na Mwandishi wetu

Akizungumza na Wananchi wanaofanya kazi katika mradi huo amesisitiza viongozi na wananchi kushirikiana katika kuhakikisha miradi inayotekelezwa na Serikali inakuwa na tija kwa jamii ili kuleta manufaa kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

Sauti ya Balozi Sirro

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Buhigwe kanali Michael Ngayalina Amesema kuwa ujenzi wa kituo hicho unatarajiwa kuongeza fursa za kiuchumi na kukuza biashara za mipakani ili kuchochea maendeleo kwa wananchi wa Buhigwe pamoja na Mkoa wa Kigoma kwa ujumla.

Muonekano wa mradi wa kituo cha pamoja cha forodha kilichopo Buhigwe, Picha na Mwandishi wetu