Joy FM
Joy FM
15 August 2026, 14:31

MV Liemba, ambayo imekuwa sehemu muhimu ya historia ya usafiri katika Ziwa Tanganyika, inatarajiwa kurejea katika huduma ikiwa ni hatua muhimu katika juhudi za serikali kuimarisha usafiri wa majini nchini
Na Mwandishi wetu
Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, amesema kuwa meli ya MV Liemba itaanza rasmi kutoa huduma za usafirishaji wa abiria kuanzia Septemba 1, 2026, baada ya kukamilika kwa ukarabati wake.
Profesa Mbarawa amesema hayo leo, Agosti 15, 2026, mjini Kigoma wakati meli hiyo ilipokuwa ikifanya majaribio yake ya kwanza katika Ziwa Tanganyika.

Amesema kukamilika kwa ukarabati wa MV Liemba na kurejea kwake katika huduma kutachochea shughuli za usafirishaji ndani ya Ziwa Tanganyika, huku serikali ikilenga kuimarisha usafiri wa majini na kuongeza ufanisi na uhakika wa safari katika Mkoa wa Kigoma.
NayeMeneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika, Edward Sylivester Mabula, amesema mradi wa upanuzi wa Bandari ya Kigoma unahusisha, miongoni mwa mambo mengine ikiwemo ujenzi na uboreshaji wa sehemu ya gati.
Baadhi ya wadau na wafanyabiashara Mkoani Kigoma wameeleza kuwa kuanza tena kwa safari za MV Liemba kutasaidia kukuza shughuli za kiuchumi na biashara katika maeneo yanayozunguka Ziwa Tanganyika.