Joy FM
Joy FM
7 July 2025, 09:39

Mkuu wa Wilaya Kasulu Mkoani Kigoma Kanali Isac Mwakisu amesema anatamani kuona mashirika yasiyo ya kiserikali yakishikamana na kufanya kazi kwa umoja katika kuwahudumia wananchi kupitia shughuli mbalimbali za kijamii
Na Emmanuel Kamangu
Mashirika zaidi ya 40 yasiyo ya kiserikal Wilayani Kasulu yametakiwa kufanya kazi kwa ushirika ili kujikwamua kiuchumi na kufanya kwa urahsi shuguli za kijamii.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kasulu kanal Isack Mwakisu akiwa katika jukwa la mashirika yasiyo ya kiserikali yanayofanya kazi zake wilayani humo ambapo amewasihi kufanya kazi kwa umoja ili kuharakisha maendeleo katika jamii.

Aidha Kanal Mwakisu ameyapongeza mashirika hayo kwa jinsi yanavyofanya kazi nzuri za kijamii huku akiahidi kuendelea kutoa ushirikiano ili kuhakikisha yanasimama imara.
Baadhi ya wa wakikilishi kutoka mashirika mbali mbali ambayo yameshiriki jukwa hili la mashirika yasiyo ya kiserikali Wilayani Kasulu wameiomba serikali kuendelea kuwashika mkono katika kuhakikisha wanapata fursa ya kujikwamua kiuchumi.
Mashirika hayo ambayo hufanya shuguli zake wilayani kasulu yameazimia kufanya kazi kwa umoja ikwa ni pamoja na kushirikishana changamoto zinazowakabili hasa kwa kipindi hiki ambacho mashirika mengi yanakabiliwa na ukata mkubwa ili kufanya vema shuguli za kijamii.