Joy FM

DED Kasulu achangia tofali 5000 ujenzi uzio wa shule

20 April 2026, 13:57

Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Kasulu Mwalimu, Vumilia Julius Simbeye akitoa hotuba katika mahafali ya wanafunzi wa kidato Cha sita katika shule ya sekondari Kigoma Grand, Picha na Hagai Ruyagila

Wazazi na walezi wametakiwa kuona umuhimu wa ushirikiano kati ya wadau wa elimu katika kutatua changamoto zinazoikabili shule ya Sekondari Kigoma Grand

Na Hagai Ruyagila

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu, mkoani Kigoma Mwalimu Vumilia Simbeye ameahidi kuchangia tofali 5000 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa uzio katika shule ya sekondari Kigoma Grand, Hatu hiyo ni sehemu ya juhudi za kuboresha mazingira ya kujifunzia pamoja na kuimarisha usalama wa wanafunzi na mali za shule.

Mwl. Simbeye ametoa ahadi hiyo wakati akijibu changamoto mbalimbali zilizowasilishwa kupitia risala ya shule, katika mahafali ya wanafunzi wa kidato cha sita yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano Samia hall shuleni hao.

Wanafunzi wa kidato Cha sita katika shule ya sekondari Kigoma Grand, Picha na Hagai Ruyagila

Aidha amewahimiza wazazi na walezi kushirikiana na uongozi wa shule kwa kuchangia maendeleo yake, hususan katika kukamilisha ujenzi wa uzio huo.

Sauti ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu

Awali akisoma risala katika mahafali hayo Mkuu wa shule ya sekondari Kigoma Grand, Mwalimu Severino Manyota, amezungumzia changamoto ya uzio na baadhi ya mafanikio.

Mkuu wa shule ya sekondari Kigoma Grand Mwalimu Severino Manyota, Picha na Hagai Ruyagila
Sauti ya Mkuu wa shule ya Kigoma Grand

Mwenyekiti wa Bodi wa shule hiyo Henry Mpabandi amemshukuru mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Kasulu kwa namna alivyoahidi kuchangia tofali hizo na kuhamasisha wazazi kuchangia shughuli za maendeleo.