Joy FM
Joy FM
13 June 2026, 15:21

Serikali imewaasa kina mama kuambatana na wenza wao wanapoenda kliniki ikiwa ni mojawapo ya mkakati wa kujabiliana na vifo vya watoto
Na Emmanuel Kamangu
Wenza katika Halmashauri ya mji wa kasulu wametakiwa kushiriki kikamilifu kiliniki ya baba na mama ili kukabiliana na vifo vya mama na mtoto vinavyoweza kujitokeza baada na kabula ya kujifungua.
Wito huo umetolewa na Bi. Sarafina Chonko ambaye ni mkunga kutoka kituo cha afya kiganamo halmashauri ya mji wa kasulu kwa niaba ya mratibu wa kukabiliana na vifo vya mama na mtoto ambapo amesema kuna kila sababu wenza kuwasindikiza wajawazito kiliniki ili kupewa njia bora ya kuendelea kumtunza kiafya mama mjazito .
Aidha Bi. Kachonko amebainisha kuwa wanaendelea kuchukua hatua mbali mbali za kiafya kwa mama mjamzito ili kuhakikisha anakuwa salama kabla na baada ya kujifungua ikiwa ni kukabiliana na vifo vya mama mtoto

Hata hivyo Bi Kachonko amesema wenza wanatakiwa kutambua dalili za hatari kwa mama mjamzito na baada ya kujifungua kwani hii itasaidia kuendelea kuimalisha usalama wa mama na mtoto alieko tumboni.
Kituo cha afya kiganamo hutuoa huduma kwa wajawazito zaidi ya miatatu kila mwezi ikitajwa ongezeko hili ni kutokana na elimu ya afya ya uzazi inayoendelea kutolea na watalamu wa afya kwa wananchi.