Joy FM
Joy FM
5 May 2025, 15:17

Halmashauri ya Mji wa Kasulu Mkoani Kigoma imevuka lengo la ukasanyaji wa mapato ya ndani kwa asilimia 102.
Na Hagai Ruyagila
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mji Kasulu mkoani Kigoma limempongeza Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Mwl, Vumilia Simbeye kwa kuvuka malengo ya ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa asilimia 102 sawa na zaidi ya Bilioni 2 na milioni 263 ya makisio na makadilio kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Mji Kasulu Mh, Selemani Kwirusha ametoa pongezi hizo katika mkutano wa baraza la madiwani katika robo ya tatu kipindi cha Januari mpaka Machi kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Halmashauri hiyo mpaka sasa imekusanya zaidi ya shilingi bilioni 2 na milioni 263 sawa na asilimia 102 ambapo mapato hayo yatasaidia katika shughuli za maendeleo kwa sekta ya elimu, afya na miundombinu ya barabara.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Mwl, Vumilia Simbeye amesema mapato hayo yameongezeka kwasababu ya umakini wa ukusanyaji wao wa mapato.
Baadhi ya madiwani wanaeleza siri ya wao kuvuka malengo ya ukusanyaji wa mapato hayo kabla hata ya mwaka kutamatika hatua ambayo imekuwa changamoto katika halmashauri nyingine wao wamewezaje.
Na hapa Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Kasulu Mwl, Vumilia Simbeye anatoa wito kwa wafanyabiashara na wananchi wa Mjini Kasulu kuona namna ambavyo suala la kodi haliepukiki maana shughuli za miradi ya maendeleo zinatokana na kodi wanazozitoa.