Joy FM

Madiwani waagiza serikali kukarabati barabara Kasulu

8 May 2026, 13:12

Madiwani wa halmashauri ya Mji Kasulu wakiwa katika kikao cha robo tatu ya mwaka wa fedha 2025/2026, Picha na Hagai Ruyagila

Ukarabati wa barabara ni msingi muhimu wa maendeleo ya taifa kwa sababu unaongeza ukuaji wa uchumi, huboresha huduma za jamii, na kuinua maisha ya wananchi

Na Hagai Ruyagila

Madiwani wa kata za Murusi, Mganza, Herujuu na Murufiti katika halmashauri ya Mji Kasulu Mkoani Kigoma wameiomba serikali kuchukua hatua za haraka kukarabati miundombinu ya barabara ambazo zimeharibika nyakati za mvua ili kuwawezesha wananchi katika shughuli za usafiri na usafirishaji wa mazao.

Katika kikao cha baraza la madiwani cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2025/2026 cha halmashauri ya Mji Kasulu Diwani kata ya Murufiti Jackson Mpombenye, diwani wa kata ya Murusi Elisha Bakena pamoja na diwani wa kata ya Mganza Abas Digimba wamesema barabara nyingi zimeharibika na kuchelewa kufanyiwa matengenezo hali ambayo imekuwa kero kwa wananchi, hasa katika maeneo yanayotegemea barabara hizo kwa shughuli za biashara, kilimo na usafirishaji wa mazao.

Sauti ya Madiwani
Madiwani wa halmashauri ya Mji Kasulu wakiwa katika kikao cha robo tatu ya mwaka wa fedha 2025/2026, Picha na Hagai Ruyagila

Akitolea ufafanuzi kuhusu barabara hizo, Kaimu meneja wa Wakala wa Barabara za Vijiji na Mijini (TARURA) Wilaya ya Kasulu Mhandisi Eric Raban, amekiri kuwepo kwa changamoto ya ubovu wa barabara hizo na kusema kuwa serikali tayari imepokea na itaendelea na mipango ya ukarabati kwa awamu kulingana na upatikanaji wa bajeti, huku akibainisha kuwa tayari baadhi ya barabara hizo zimeanza kukarabatiwa.

Sauti ya Mhandisi Eric Raban
Kaimu meneja wa TARURA wilaya ya Kasulu Injilia Eric Raban, Picha na Hagai Ruyagila

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kasulu Mh. Ayubu Ngalaba, amemshauri Meneja wa TARURA kuchukua hatua za dharura kwa kuweka bajeti nyingine kwa barabara zilizoharibiwa na TANROAD wakati wa ujenzi wa barabara kuu ya Kasulu kuelekea Kibondo ili fedha za matengenezo kutoka TANROAD zitakapotolewa ziweze kufanya kazi nyingine

Sauti ya Mwenyekiti halmashauri.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji Kasulu Mh Ayubu Ngalaba, Picha na Hagai Ruyagila