Joy FM

Mradi wa umeme wa jua kuchochea uchumi Kigoma

26 November 2026, 20:30

Hapa ni katika mradi wa kuzalisha umeme wa jua katika eneo la KISEZ Manispaa ya Kigoma Ujiji, Picha na Mwandishi wetu

Serikali imesema inaendelea kusimamia na kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji ili kusaidia kuchea mawndeleo na kukuza uchumi

Na Mwandishi wetu

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, amesema uwekezaji wa mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia nishati ya jua (Sola) ni hatua muhimu katika kukuza uchumi na kuongeza upatikanaji wa nishati jadidifu nchini.

Profesa Mkumbo amesema uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Serikali katika kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji, kuongeza uzalishaji wa nishati na kuchochea shughuli mbalimbali za kiuchumi kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

Waziri Kitila Mkumbo akiwa ameambatananna viongozi mbalimbali wakati alitembelea mradi wa kuzalisha umeme wa jua Manispaa ya Kigoma Ujiji, Picha na Mwandishi wetu

Amesema matumizi ya nishati jadidifu, ikiwemo nishati ya jua, yana nafasi kubwa katika kuongeza vyanzo vya umeme na kusaidia maendeleo ya sekta mbalimbali za uzalishaji.

Muonekano wa sola katika mradi wa kuzalisha umeme wa jua, Picha na Mwandishi wetu

Kwa upande wake, msimamizi wa mradi huo wa umeme wa Sola amesema mradi huo una uwezo wa kuzalisha megawati tano (5) za umeme, hatua itakayoongeza mchango wa nishati ya jua katika uzalishaji wa umeme.