Joy FM

Milioni 580 kutekeleza miradi ya maendeleo Kasulu

19 October 2026, 15:14

Kaimu Mkurugenzi halmashauri ya Mji wa Kasulu, Picha na Hagai Ruyagila

Serikali imeendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu

Na Hagai Ruyagila

Halmashauri ya Mji Kasulu imepokea kiasi cha shilingi milioni 580 kwa ajili ya kuendeleza shughuli za maendeleo.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Kasulu Nurfus Aziz Ndee ambaye amesema fedha hizo wamepokea kutoka serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa nyumba mbili za wakuu wa Divisheni/Vitengo, ukamilishaji wa nyumba moja ya Mkurugenzi, ukamilishaji wa nyumba mbili za Maabara, ununuzi wa vifaa tiba pamoja na fedha za ufuatiliaji na tathmini kwa miradi husika kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

Aidha ameishukuru serikali kwa namna inavyotimiza wajibu wake kwa halmashauri hiyo katika shughuli za maendeleo katika sekta mbalimbali ndani ya halmashauri hiyo.

Muonekano mradi wa nyumba, Picha na Hagai Ruyagila

Baadhi ya wananchi wa halmashauri hiyo wamesema ni vizuri fedha hizo zikatumika kwa maelekezo yaliyotolewa na serikali ili kufanikisha miradi hiyo.

Hata hivyo, Serikali imeendelea kutoa fedha katika halmashauri mbalimbali hapa Nchini kwa ajili ya kufanikisha miradi ya maendeleo inakamikika kwa wakati.