Joy FM
Joy FM
16 November 2026, 16:04

Wananchi wametakiwa kushirikiana na vyombo vya dola kutoa taarifa za uhalifu na vitendo vya ukatili ili hatua stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa.
Na Josephine Kiravu
Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma limefanikiwa kukamata madereva na kubaini makosa 9,499 ya usalama barabarani na kutoza faini huku madereva 7 wa pikipiki wakiwa wamefikishwa mahakamani na madereva 3 wakifutiwa leseni.
Akizungumza na wanahabari hii leo Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani Kigoma SACP Filemon Makungu amesema oparesheni hiyo ni endelevu na kuwataka madereva kuzingatia na kutii sheria za usalama barabarani.

Katika hatua nyingine jeshi la Polisi limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa zaidi ya 5 katika wilaya ya Kibondo na Uvinza kwa kujihusisha na matukio ya wizi na kumiliki mali zinazodhaniwa kuwa za wizi.
Aidha katika kuhakikisha vitendo vya ukatili vinatokomezwa kwenye jamii, Mahakama ya wilaya ya Kasulu imemhukumu kifungo cha kwenda jela miaka 30 mshitakiwa Vicent Wilson Nsumira mwenye umri wa miaka 21 baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kubaka mwanafunzi mwenye umri wa miaka 17.