Joy FM
Joy FM
2 November 2026, 17:04

Mkuu wa Wilaya Uvinza Mkoani Kigoma Mh. Mtela Mwampamba amesema kuwa wazazi na walezi hawana budi kushirikiana na serikali katika kuhakikisha watoto wanapata chakula wakiwa shuleni
Na Orida Sayon
Wazazi na walezi katika Halmashauri ya Wilaya Uvinza Mkoani Kigoma wameshauriwa kuchangia chakula ili watoto wote wapate chakula wawapo shuleni ili kudhibiti utoro na wanafunzi kufeli mitihani yao.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mhe. Mtela Alam Mwampamba wakati akizungumza na wanafunzi na baadhi ya wazazi na walezi katika hafla ya mahafali ya pili ya kidato cha nne na darasa la pili (kindagaten 2) katika shule ya kandahari iliyopo kata ya kazuramimba wilayani uvinza.

Mwampamba amesema kila mzazi au mlezi ana wajibu kumpatia mtoto chakula hivyo mzazi/mlezi atakayevunja sheria ya kuchangia chakula atapewa adhabu ya kulipa kiasi cha shilingi laki tano za kitanzania au kwenda gerezani kwa muda wa miezi 6 huku akiahidi kusimamia sheria hiyo.
Mhe. Mwampamba amesema katika kufanikisha urahisi wa upatikanaji wa chakula taasisi zote za umma na kila shule kuwa na bustani za mbogamboga na matunda itakayosimamiwa na wanafunzi wa shule husika.

Baadhi ya wazazi wakaeleza mtazamo namna uchangiaji wa chakula unavyoweza kuasidia watoto wao wawapo shuleni na hatua hiyo itasaidia kuinua kiwango cha ufaulu shuleni.