Joy FM

Wanavyuo Kasulu waaswa kutumia mitandao kujipatia kipato

29 October 2026, 11:48

Wanachuo wa huo cha FDC Kasulu wakiwa kwenye picha na Mkuu wa Polisi jamii Wilaya Kasulu ASP Masangora Kitina

Maendeleo ya teknolojia na mawasiliano imeendelea kukua kwa kasi na hivyo kuongeza matumizi ya mitandao ya kijamii miongoni mwa jamii na matumizi chanya yanaweza kuongeza fursa na kipato kwa vijana hasa wananvyuo

Na Hagai Ruyagila

Wanafunzi wa Chuo cha FDC Kasulu kilichopo katika Halmashauri ya Mji Kasulu, Mkoani Kigoma, wametakiwa kutumia mitandao ya kijamii kama fursa ya kujipatia kipato na kukuza maendeleo yao, badala ya kuitumia katika vitendo vinavyokiuka maadili ya jamii.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Polisi Jamii wa Wilaya ya Kasulu, ASP Masangora Kitina, wakati wakizungumza na chuo hao, ambapo ametoa elimu kuhusu matumizi sahihi na yenye tija ya mitandao ya kijamii kwa wanafunzi hao.

Polisi kata wa Kata ya Nyamnyusi Willy Lupa, Picha na Hagai Ruyagila

Kwa upande wake, Polisi Kata wa Nyamnyusi, Willy Lupa, amewasisitiza Wana chuo hao kuwa wazalendo na watiifu kwa taifa lao, akieleza kuwa misingi hiyo ni muhimu katika kuwajenga kuwa viongozi bora wa sasa na wa baadaye. 

Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha FDC Kasulu wamesema matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na ukosefu wa elimu kuhusu namna sahihi ya kutumia majukwaa hayo.

Kutokana na hali hiyo, wamehimiza kuendelea kutolewa kwa elimu kwa jamii ili kuongeza uelewa kuhusu matumizi salama na yenye manufaa ya mitandao ya kijamii.