Joy FM
Joy FM
19 October 2026, 10:48

Serikali imeendelea kuhamasisha matumizi ya mkaa mbadala lengo likiwa ni kuhakikisha wananchi wanaepukana na uharibifu wa mazingira
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi (Muungano na Mazingira) Mhandisi Hamad Yusufu Masauni, ameipongeza Halmashauri ya wilaya ya Kakonko kwa jitihada wanazofanya katika kuhamasisha wananchi kutumia nishati safi.
Pongezi hizo amezitoa katika Ukumbi mpya wa Halmashauri ya wilaya ya Kakonko.
Mh. Waziri Masauni ametembelea Mradi wa Mazingira wa Kiwanda cha Mkaa mbadala na kuona jitihada za Kiwanda hicho juuu ya kupunguza athari za uchafunzi wa Mazingira na kuchukua taka kama fursa ya biashara na kutumia kama nishati safi kwa matumizi ya ya binadamu na kutokomeza kukata miti hovyo na kuharibu mazingira

“Ni lazima tufanye vitu kwa faida ya Maisha yetu ya Kila siku, uharibifu wa Mazingira huathiri tabia ya Nchi ikiwemo kilimo,mifugo,maji na mazingira pamoja na maisha ya Kila siku” Mh. Masauni amesema.
Kanali Evance Malassa, Mkuu wa wilaya ya Kakonko amesema wilaya inaendelea kutoa jitihada mbali mbali za wananchi kutumia nishati safi licha ya changamoto zilizopo za kukata miti na uchomaji misitu Bado wilaya imesimama kidete kupambana na vitendo hivyo, pia amesema wananchi wapo teyari kulinda mazingira kwa vitendo na kbiashara kwa ujumla.

Mh. Waziri Masauni yupo katika ziara ya kikazi mkoani Kigoma ambapo ameanza ziara yake kwa kutembelea Wilaya ya Kakonko na kuona jitihada za Mradi wa Mkaa mbadala
