Joy FM
Joy FM
6 November 2026, 17:34

Wataalamu wa mifugo Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma wametakiwa kuboresha utoaji qa guduma bora kwa wafugaji wa mifugo
Na Mwandishi wetu
Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mh. Mtela Mwampamba , ametoa maelekezo mbalimbali kwa Wataalamu wote wa Mifugo ili kuboresha utoaji wa huduma Bora kwa wafungaji wa mifugo.
Akizungumza wakati ufunguzi wa mafunzo ya Wataalamu wa mifugo, Mh. Mwampamba amewataka kutokusababisha migogoro kati ya wakulima na wafugaji kwa kufuata miongozo yote ya kazi na kuweza kutatua kwa wakati.

Kwa upande mwingine, Mh. Mwampamba amewaomba kusimamia vyema ukusanyaji wa mapato kwa kuziba mianya ya upotevu wa mapato yatokanayo na uzalishaji wa mifugo ndani ya Wilaya ya Uvinza na namna Bora ya kuhesabu mifugo inayoingia na kutoka kwenye minada, pia amewataka kutafuta namna ya kuanzisha huduma ya nyama choma kwenye minada ili wananchi waweze kupata kitoweo ndani ya maeneo hayo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Ndg. Japheth Njawala amewataka wataalamu kutekeleza majukumu yao na kufuata Sheria zote za kuingiza na kutoa mifugo ndani na nje ya nchi.Pia amesisitiza kama kuna changamoto yoyote watoe taarifa kwa wakati.Vile vile amewataka kuendelea na zoezi la kuchanja ng,ombe dhidi ya ugonjwa wa mapafu.