Joy FM
Joy FM
20 November 2026, 15:52

Ubunifu unaweza kusaidia sana wahitimu wa vyuo vikuu kwa kuwapatia njia mpya za kujiajiri, kutatua changamoto za jamii na kujenga maisha bora badala ya kutegemea ajira za kuajiriwa pekee
Na Mwandishi wetu
Wakufunzi wanaohitimu katika taasisi ya uhasibu Tanzania TIA Mkoa wa Kigoma wametakiwa wabunifu wabunifu ili kuendana mabadiliko ya sayansi na teknolojia kutokana soko la ajira duniani kwani ulimwengu unahitaji ubunifu kuliko masomo ya darasani.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya Kigoma Dkt. Rashid Chuachua kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro katika mahafari ya 24 ya chuo cha uhasibu Tanzania ambayo yamefanyika katika chuo hicho kampasi ya Kigoma ambapo jumla ya wanachuo 587 wamemaliza Masomo katika fani mbalimbali.

Dkt. Chuachua amesema kuna kila sababu ya vijana wanaomaliza katika Chuo hicho kuwa chachu ya Maendeleo katika Mkoa wa Kigoma kutokana na Mkoa wa Kigoma kuwa kimkakati hivyo wanatakiwa kuchochea shughuli za kiuchumi na biashara kukua katika mkoa huo

Naye Mtendaji Mkuu wa Chuo Cha Uhasibu Tanzania William Palangyo pamoja na mambo mengine amesema Serikali kukamilisha ujenzi wa chuo hicho kwa zaidi ya shilingi bilioni 11 wamesaidia kuongeza udahili wa Wanachuo wanaojiunga na Chuo hicho.
Baadhi ya wanachuo wamesema watahikikisha wanakuwa waaminifu katika jamii nakutumia elimu waliopita kuwa wabunifu nakuweza kushindana katika soko la ajira nakuweza kujiajiri wenyewe bila kutegemea ajira kutoka Serikalini