Joy FM

Mitandao ya kijamii yageuka nuru kwa wanawake wafanyabiashara Kigoma

20 November 2026, 17:43

Wanawake wakifurahia uendeshaji wa biashara mtandaoni, Picha na Joy Fm

Mitandao ya kijamii ni nyenzo muhimu katika kukuza biashara endapo itatumiwa vizuri

Na Timotheo Leonard

Baadhi ya wanawake wafanyabiashara Mkoani Kigoma wameitaja mitandao ya kijamii kama ukombozi mkubwa uliobadilisha maisha yao, kwa kuwawezesha kujiingizia kipato na kutangaza bidhaa zao kwa wateja wengi ndani na nje ya nchi.

Ukuaji wa teknolojia na matumizi ya intaneti nchini Tanzania unaendelea kufungua milango ya kiuchumi kwa wananchi wengi, kwa mujibu wa  ripoti ya hivi karibuni ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa mwaka wa fedha wa 2025/2026, inaonyesha kuwa usajili wa watumiaji wa intaneti nchini umekua kwa kasi kubwa na kufikia zaidi ya milioni 58.9.

Sauti za wanawake

Kasi hii inachangiwa kwa kiasi kikubwa na ongezeko la wananchi, hasa wanawake, wanaotumia simu janja  ambazo zimefikia milioni 29.8 nchini, kujiingiza kwenye biashara za mtandaoni ili kujikwamua kiuchumi.

Veronica Biaka na Siri Jumanne Rajabu, ni miongoni mwa wanawake mkoani Kigoma wanaonufaika na mifumo hii. Wanasema mitandao ya kijamii inawarahisishia kufanya biashara wakiwa eneo lolote, bila kulazimika kukaa sehemu moja kusubiri wateja.

Sauti ya wanaume

Licha ya wanawake hawa kuendelea kunufaika kupitia mitandao ya kijamii, wanaume mkoani humo nao hawapo nyuma katika kuchamkia fursa hiyo ya soko la kidijiti, kama anavyoeleza Adamu Sadick.

Ili kuhakikisha wajasiriamali hawa wanatumia mtandao kwa tija na usalama, Serikali kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii imekuwa ikichukua hatua madhubuti kama anavyoeleza Raban Gwaguzo, ambaye ni Afisa Maendeleo  Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Sauti ya afisa maendeleo ya jamii