Joy FM

Wazazi, walezi waonywa kuficha watoto wenye ulemavu Kigoma

29 October 2026, 08:43

Kwenye picha ni watoto wenye ulemavu tofauti tofauti, Picha na Joy Fm

Watoto wenye ulemavu wana haki ya kupata elimu na kushiriki katika shughuli mbalimbali kama watoto wengine

Na Josephine Kiravu

Wazazi na walezi Mkoani Kigoma wametakiwa kuacha kuwafungia ndani watoto wenye ulemavu badala yake wapelekwe shuleni kwa ajili ya kupata elimu na ujuzi kwenye fani mbalimbali.

Hayo yamejiri wakati wa zoezi la utoaji elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kumpatia haki ya elimu mtoto mwenye ulemavu.

Akizungumza  wakati wa zoezi hilo Afisa elimu maalum Manispaa ya Kigoma Ujiji  Ezekiel John amesema kupitia wadau mbalimbali mwitikio wa kuandikisha watoto wenye ulemavu ni mkubwa na kuwataka wazazi kuacha kusingizia kipato kidogo kuwa chanzo cha kushindwa kupeleka watoto shule.

Sauti ya Afisa elimu maalumu

Naye  Mwezeshaji masuala ya elimu kwa wototo wenye ulemavu kutoka Chama cha Viziwi Tanzania kupitia mradi wa Haki ya elimu kwa watoto wenye ulemavu Dkt. William Henry Kitila amesema wanatarajia kuifikia jamii kwa kuwapatia elimu ili kuondoa unyanyapaa kwa watoto wenye ulemavu.

Sauti ya Dkt. William Henry Kitila

Kwa mujibu wa chama cha viziwi Tanzania watoto wenye ulemavu hukwama kimasomo si kwa kupenda bali kwa vikwazo vya umasikini na dhana potofu kuwa wao ni mzigo.

Hata hivyo chama hicho wameendelea kutoa elimu kupitia mikutano ya hadhara kwenye maeneo ya sokoni.