Joy FM

Wananchi wataka elimu utambuzi dawa bandia Kigoma

23 October 2026, 14:37

Baadhi ya dawa bandia ambazo zimekamatwa na TMDA Kanda ya Magaharibi

Matumizi ya dawa bandia yametajwa kuwa hatari zaidi kwa afya ya binadamu na hivyo mamlaka husika zimetawakiwa kuwachukulia hatua za kisheria wanaendelea kuuza dawa hizo bandia

Na Josephine Kiravu

Wananchi Mkoani Kigoma wameitaka Serikali kuwapatia elimu ya kutambua dawa bandia na zisizofaa kwa matumizi ya wanadamu na wanyama zinazouzwa kwenye maduka ya dawa muhimu za binadamu na mifugo ili kulinda afya zao.

Wakizungumza mara baada ya mkutano wa wanahabari na meneja wa TMDA kanda ya magharibi, wananchi hao wamesema taasis hiyo inapaswa kutumia majukwaa ya mitandao ya kijamii na mikutano ili kutoa elimu ya utambuzi wa dawa.

Miongoni  mwa wananchi hao ni Richard Gaspa mkazi wa Kibirizi na Irene Abeli mkazi wa Airport wmekiri kutokuwa na uelewa wa namna ya kutambua dawa bandia na kuwa hali hiyo inaweza kuhatarisha maisha ya wananchi wengi endapo hawatapatiwa elimu.

Kwa upande wake Meneja wa TMDA kanda ya Magharibi Christopher Migoha amesema wamefanikiwa kukamata dawa na kuziondoa sokoni zenye thamani ya zaidi ya shilingi million 5 na nusu katika wilaya ya kigoma na Kasulu.

Hata hivyo amewataka wananchi kuhakikisha wananunua dawa kwenye maduka ya dawa muhimu kulingana na maelezo ya daktari ili kupunguza usugu wa dawa huku akiwataka pia watoa huduma kutoa huduma kwa wananchi kulingana na taratibu na sheria zilizowekwa.