Joy FM
Joy FM
7 October 2026, 14:15

Ushirikiano wa mashirika yasiyo ya serikali, wadau pamoja na serikali ndio nguzo muhimu ya kusaidia kukuza na kuongeza utoaji wa huduma kwa wananchi.
Serikali Mkoani Kigoma imeyataka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) kuboresha huduma, kuongeza ubunifu na kuungana na serikali katika kusukuma maendeleo kwa wananchi ili kufikia malengo ya dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Mhe. Dkt. Rashid Chuachua, ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Balozi Simon Siro, katika Jukwaa la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali lililoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kwa kushirikiana na Mradi wa Pamoja wa Umoja wa Mataifa Kigoma (UN Kigoma Joint Program)
Naye mratibu wa Jukwaa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ambaye ni Afisa Maendeleo wa Mkoa wa Kigoma, Bw. Msafiri Nzuruni, amesema jukwaa hilo limewakutanisha mashirika mbalimbali kutoka mkoa mzima kwa lengo la kujadili namna ya kuwainua wananchi kiuchumi.

Kwa upande wake, Mratibu wa Mradi wa Pamoja wa Umoja wa Mataifa Mkoa wa Kigoma unaofadhiliwa na nchi za Ireland na Norway, Bw. Daniel Nicas Muyabhaga, amesema wataendelea kushirikiana ili kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa ufanisi zaidi.
Aidha, Jukwaa hilo la mwaka huu limeongozwa na kaulimbiu isemayo: “Fikra Mpya Kuhusu Uendelevu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali: Ubia na Upatikanaji wa Rasilimali Fedha Kupitia Vyanzo vya Ndani”.