Joy FM

DC Uvinza ataka ulinzi wa watoto dhidi ya ukatili

5 November 2026, 11:56

Mkuu wa wilaya ya Uvinza Mhe, Mtella Allam Mwampamba, Picha na Orida Sayon

Licha ya hamasa na elimu kuendelea kutolewa kwa wananchi mkoani kigoma kuhusu vitendo vya ukatili bado vitendo hivyo vimeendelea kuripotiwa kwa baadhi ya maeneo ambapo watoto ni miongoni mwa kundi kubwa linalokumbana na vitendo hivyo vya ukatili

Na Orida Sayon

Wito umetolewa kwa wazazi na walezi Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vya ukatili na kutoa taarifa unapotokea ukatili katika maeneo yao.

Ukosefu wa, mawasiliano mazuri kati ya wazazi na maendeleo ya teknolojia bila ya uangalizi wa watoto vinatajwa kuwa miongoni mwa sababu za ukatili kwa watoto huku watu wa karibu wakitajwa kuwa miongoni mwa watu wanaotekeleza vitendo hivyo ambapo Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mhe, Mtella Allam Mwampamba amewataka wazazi kuzingatia wajibu wa kuwalinda watoto.

Sauti ya DC Mwampamba

Aidha Mwampamba amewataka wazazi/walezi na jamii kuwa sehemu ya kumlea mtoto katika malezi chanya yanayomuandaa kukabiliana na majukumu ya badae kulingana na mila na desturi za kitanzania.

Sauti ya DC Mwampamba

Nao baadhi ta wazazi na walezi wamesema watoto wote wa kike na kiume wanapaswa kulindwa sawa huku wakihiza kuwajibaka kuwapatia mahitaji yao kuwalinda dhidi ya vishawishi vinavyoweza kupelekea kuingia kwenye mtego wa ukatili.

Sauti ya Wazazi Mtoto ni nguvu kazi ya taifa