Joy FM

Mayeye CUP yaanza kurindima Kigoma DC

2 September 2026, 13:42

Baadhi ya wachezaji wa timu ya Kamala Fc wakiwa tayari kwa michezo, Picha na Sadick Kibwana

Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini mkoani Kigoma ameanzisha mashindano ya mpira wa miguu yenye lengo la mashindano hayo ni kukuza vipaji na kudumisha mshikamano miongoni mwa jamii.

Na Sadick Kibwana

Ligi ya mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Mhe. Kiza Mayeye (Mayeye Cup), imeanza rasmi Jumanne hii, Septemba 1, 2026, katika uwanja wa tarafa ya Mwandiga ikihusisha jumla ya timu 32.

Baadhi ya wachezaji wakiwa tayari kwa mechi, Picha na Hagai Ruyagila

Akizungumza kwa niaba ya Mbunge huyo, Katibu wa Mbunge, amesema lengo la ligi hiyo ni kuwapa fursa vijana kwa kukuza vipaji, kuonekana, na kujipatia kipato.

Sauti ya Katibu wa Mbunge

Aidha, Mwenyekiti wa Mashindano hayo, Bw. Dotto Kondo, amesema ligi hiyo inaanza kwa kuhusisha timu zilizo ndani ya jimbo hilo pekee lenye kata 16.

Naye Katibu wa chama cha soko Wiliya Kigoma DOKFA, Dumango Yahaya amepongeza mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini Kiza Mayeye kwa kuanzisha mashindano hayo ambayo yatasaidia kuibua vipaji kwa vijana mbali na kuleta mshikamano kwa wananchi wa jimbo hilo.

Sauti ya Katibu wa chama cha soko Wiliya Kigoma DOKFA, Dumango Yahaya

Ligi ya Mayeye Cup 2026 inafanyika kwa mara ya kwanza tangu mbunge huyo apate nafasi ya kuongoza Jimbo la Kigoma Kaskazini, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi alizozitoa kwa vijana wa jimbo hilo. 

Wachezaji wakifanya mazoezi kabla ya mchezo kuanza, Picha na Sadick Kibwana